Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda Awadhi: Askari tendeni haki

FB IMG 1661664922322 Kamanda Awadhi

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP Awadhi Haji amewataka askari wa Jeshi la Polisi nchini kutenda haki kwa wananchi na kutoa huduma bora kwa wananchi wanao wahudumia ili kujenga imani kwa wananchi juu ya Jeshi lao.

Kamishina Awadhi amesema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha ambapo amewataka viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani humo kusimamia vyema maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ambayo aliyatoa mara tu alipopewa dhamana na amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuliongoza Jeshi la Polisi nchini.

Aidha, CP Awadhi alipata wasaa wa kutembelea kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia mkoani humo ambapo amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii hivyo amewataka askari kutoa huduma bora kwa watalii wanaofika nchini ili kuleta maana halisi ya Tanzania The Royal Tour ambayo ilizinduliwa mapema mwaka huu na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live