Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaka asimulia alivyonusurika ajalini, ilivyoua bibi harusi na wenzake

63852 Msibapic

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbarali. Nicolausi Mwandunga ambaye ni kaka wa aliyekuwa bibi harusi, Diana Mwandunga amesimulia jinsi ajali ilivyoua ndugu zake wanne na kujeruhi wawili akiwamo yeye mwenyewe.

Diana aliyekuwa mchumba wa Elisante Edward  ambao walikuwa waoane leo Jumamosi ya Juni 29, 2019 alifikwa na mauti Jumatano iliyopita asubuhi Juni 19, 2019 katika ajali ya gari dogo kwenye eneo maarufu kwa jina Machimbo, Barabara Kuu ya Mbeya-Makambako na kusababisha vifo hivyo.

Wengine waliofariki dunia ni Faraja Mwandunga, James Mwandunga na mtoto wa Faraja, Jacton (2) wakati waliojeruhiwa ni Ibrahimu Mwandunga na Nicolausi Mwandunga.

Wana ndugu hao walifikwa na mauti wakati wakitoka nyumbani kwao Chimala kulikofanyika sherehe ya kumuaga Diana ‘send off’ iliyofanyika Juni 15, 2019.

Akizungumza na Mwananchi jana Ijumaa Juni 21, 2019 kuhusu mazingira ya ajali ilivyokuwa, Nicolausi ambaye alikuwa amekaa mbele alisema waliondoka Chimala saa 11:14 alfajiri   kwenda jijini Dar es Saalam na walisafiri takribani kilomita 35 kabla ya kupata ajali hiyo.

Alisema walipofika eneo la Machimbo barabara Kuu  ya Mbeya-Makambako  walikuta malori mawili mbele yao yakiwa yameharibika barabarani  na bahati mbaya hakukuwa na alama yoyote inayoonesha mbele kuna magari yameharibika.

Habari zinazohusiana na hii

“Sasa nyuma ya hayo malori yaliyokuwa yameharibika kulikuwa na Fuso na zote zilikuwa upande wao, hivyo nadhani yule mwenye Fuso alifikiri zile lori mbili zilikuwa zinatembea kwa vile hakukua na alama yoyote ile,” alisema Nicolausi

“Hivyo alivyozikaribia zaidi na kubaini kuwa zimesimama ndio akaamua kuchepuka na kuja upande wetu sisi kwa maana ya upande wa gari zinazotoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam. Sasa  na sisi tulikuwa tumeishakuwa  katikati ya usawa wa zile lori mbili, hivyo  dereva wetu alipoona mwenye Fuso ameingia upande wetu akaamua kuikwepesha gari ili asigongane uso kwa uso.”

Kaka huyo alisema, “Lakini vile dereva wa Fuso alikuwa mwendo kasi na tayari alikuwa ameshatufikia akaigonga gari letu kuanzia usawa wa mlango wa nyuma wa abiria.”

Alisema nyuma ya gari yao ndio walikokuwapo wadogo zake watatu ambao wote walipoteza maisha papo hapo baada ya kugongwa na baada ya kupigwa gari yao ikahama kabisa barabara na baada ya hapo yeye na dereva (Ibrana) hawakujua kilichoendelea kwa vile walipoteza fahamu wakaja kushtuka wapo Hospitali ya Wilaya ya Mbarali.

 

Kwa undani wa simulizi ya kaka mwingine wa Diana, bwana harusi mwenyewe Elisante akimwelezea Diana na jinsi walivyoanzisha mahusiano yao, alivyopokea taarifa za kifo, soma nakala ya Mwananchi leo Jumamosi Juni 22, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz