Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera yajipanga kuiduwaza Yanga

02de1e738ebebaf6a036aefa2d76da2e Kagera yajipanga kuiduwaza Yanga

Thu, 17 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime amewaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Yanga unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba huku akiahidi kuwaduwaza mabingwa hao wa kihistoria.

Kagera haijapata matokeo mazuri tangu imeanza msimu mpya ndani ya mechi mbili walizocheza wametoka sare moja dhidi ya Gwambina FC, na mwingine kufungwa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Akizungumza kwa simu kutoka Bukoba jana, Maxime alisema amechoka kuona kikosi chake kinapata matokeo mabaya, hivyo amekipanga kikosi chake kiushindani ili kuchomoza na ushindi dhidi ya Yanga.

“Mchezo utakuwa na ushindani kwani kila timu itahitaji ushindi, lakini kwetu tumechoka kupata matokeo yasiyoridhisha nawaomba mashabiki waje kwa wingi kupokea ushindi,” alisema Maxime.

Alisema licha ya Yanga kuwa na historia ya kupata ushindi kila wanapokutana kwenye uwanja huo, safari hii amejipanga kuvunja mwiko huo wa kufungwa na Yanga.

“Mchezo wa mpira hauna kitu cha ziada zaidi ya kujipanga kwa mbinu za kukabiliana na wapinzani wetu, kwa kuwa tunawajua baada ya kuwaangalia kwenye mechi zao kadhaa walizocheza," alisema Maxime.

Alisema wataingia kwenye mchezo huo kwa nidhamu kubwa kwa kukiheshimu kikosi cha Yanga, sawa na timu 17 zinazoshiriki ligi hiyo msimu wa mwaka 2020/2021.

Chanzo: habarileo.co.tz