Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaburi lafukuliwa, jeneza lawekwa mlangoni

Kaburi Lafukuliwa, Jeneza Lawekwa Mlangoni.png Kaburi lafukuliwa, jeneza lawekwa mlangoni

Wed, 18 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni tukio la kushangaza. Ndivyo unavyoweza kuelezea kile kilichotokea katika familia ya Venant Zabron (52), Mkazi wa Kahinga, Kata Bugomola, wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera baada ya kaburi la mjukuu wake kufukuliwa na watu wasiojulikana.

Mbali na kufukuliwa kwa kaburi hilo, watu hao walichukua jeneza lilokuwa na mwili wa mtoto huyo, Faston Innocent (1) na kulitekeleza mlangoni mwa nyumba ya Zabron. Tukio hilo lililotokea jana Jumanne, Septemba 17, 2024 limeibua taharuki kijijini hapo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Septemba 18, 2024, Zabron amesema jana saa 12 asubuhi akiwa ndani ya nyumba yake, alisikia kelele za majirani waliokuwa wakipita kwake, lakini hawakubaini chanzo.

Amesema walipotoka nje waliona jeneza hilo liliokuwa na mwili wa marehemu mjukuu wake waliyemzika siku chache zilizopita likiwa nimefunuliwa mlangoni, huku mashuka na msalaba vikiwa eneo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe amesema amepokea taarifa za awali kuhusu tukio hilo na anafuatilia na baadaye atalizungumzia baada ya kupokea taarifa kamili.

"Ni tukio baya kwenye jamii na kuogopesha, ila nalifuatilia baadaye nitalizungumzia baada ya kupokea taarifa kamili," amesema mkuu huyo wa wilaya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live