Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KTO 2,100 walikatishwa masomo

896c10357085419138bb92b011c6e5da KTO 2,100 walikatishwa masomo

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAWAKE vijana zaidi ya 2,100 ambao waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali watapatiwa maarifa na stadi za maisha ili kuwakomboa kiuchumi.

Wanawake hao watakifikiwa na programu ya "Elimu Haina Mwisho" inayotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) .

Lengo la Programu hiyo ni kugusa vijana waliokuwa katika hali duni ya maisha walioathirika na ndoa za utotoni, mimba za utotoni na ukeketaji.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya KTO, Maggid Mjengwa wakati akifunga warsha ya siku tano iliyotolewa kwa walimu na waratibu wa mafunzo yanayogusa mradi huo.

"Kwa kushirikiana na Wizara husika pamoja na wadau wa elimu na washirika wa maendeleo tumekuwa pamoja katika kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika kuyafikia malengo haya na hii ni pamoja na lile la kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda" alisema.

Alisema kuwa Programu hiyo inalenga kutoa mafunzo ya sekondari, elimu ya ufundi, ujasiriamali na stadi za maisha kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi.

"Vyuo hivi vilianzishwa mwaka 1975 kwa mawazo ya baba wa taifa na vimekuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa vimekuwa vikitoa mafunzo nje ya mfumo rasmi kulingana na mahitaji ya wakati na eneo husika," alisema.

Kwa upande wake mshiriki ambaye pia ni mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Newala, Geofrey Nchimbi amesema kuwa programu hiyo hiyo inamanufaa makubwa .

Chanzo: habarileo.co.tz