Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juhudi kuzima moto hoteli ya White Sands zaendelea

14954 HOTELI+PIC TanzaniaWeb

Sat, 1 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hotel ya White Sands ya jijini Dar es Salaam inateketea kwa moto ambao bado haujaelezwa chanzo chake.

Moto huo umezuka leo jioni Ijumaa Agosti 31, 2018 na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo.

MCL Digital imefika eneo la tukio na kukuta sehemu ya jengo la hoteli hiyo likiendelea kuteketea kwa moto huku juhudi za kuuzima zikiendelea.

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi.

Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo, Joseph Paul ameieleza MCL Digital kuwa moto huo ulianza saa 10 jioni katika eneo la mgahawa, kubainisha kuwa hajui chanzo ni nini.

Chanzo: mwananchi.co.tz