Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate azungumzia uboreshaji wa uchimbaji wa madini ya Kaolin

15968 Joketi+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kisarawe. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo jana Jumatano  Septemba 5, 2018 ametembelea maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, yakiwemo maeneo ya uchimbaji wa madini ya Kaolin.

Jokate ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo na ofisa madini mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Maganga.

Katika ziara hiyo, kamati hiyo imebainisha maeneo rafiki ya uwekezaji wa shughuli za madini ambayo hayaingiliani na shughuli za binadamu ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

“Tumeamua na tutafanya, kwa kifupi Kisarawe itakua Wilaya ya kwanza kuonyeha njia ya kuvutia uwekezaji wa madini  hapa nchini,” amesema Jokate.

“Tutaanza na madini Kaolin lengo likiwa kutambua mapema maeneo na kuitangaza kimkakati kwa ajili ya wawekezaji, lakini pia kufufua mgodi mkubwa wa chini Pugu.”

Katika kuhakikisha Wilaya inatoa fursa kwa wawekezaji wa viwanda, kamati hiyo imeazimia kuweka nguvu kuhakikisha maeneo yote yenye rasilimali ya madini ya Kaolin yanabainishwa.

Jokate amesema lengo la uamuzi huo ni kuvutia wawekezaji wenye nia thabiti ya kuwekeza kwenye uchimbaji huo.

Amesema katika kutimiza hilo, Serikali itahakikisha maeneo yote yasiyofanyiwa kazi ikiwemo eneo ambalo lililokuwa na mgodi, Pugu underground mine linafufuliwa ili  kuibua fursa kwa uwekezaji na kusaidia ongezeko la mapato ya Serikali na wananchi.

Amesema Serikali imedhamiria kutumia wataalamu wa wakala wa jiolojia nchini.

Amebainisha kuwa mpango huo utasaidia kuongeza mapato ya Serikali na Halmashauri ya Kisarawe ikiwemo kufungua fursa za ajira na uchumi kwa Wilaya na Taifa,

Kwa sasa mapato yanayotokana na ushuru wa malighafi za ujenzi kama kokoto, mchanga, Kaolin kwa halmashauri hiyo kwa mwaka 2017/18 ilikuwa Sh707milioni.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz