Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate awataka wajawazito kufanya mazoezi

DC Jokate Jokate awataka wajawazito kufanya mazoezi

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amewataka Wanawake wajawazito kuzingatia lishe bora inayoambatana na kufanya mazoezi wakati wote wa ujauzito ili kulinda afya ya Mama na Mtoto itakayosaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

DC Jokate ametoa wito huo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wake Theodora Malala ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Charambe wakati wa uzinduzi wa mbio za Temeke Maternal Jogging zenye lengo la kuihamasisha jamii kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya lishe bora wakati na baada ya ujauzito utakaosaidia kujenga kizazi bora, uliofanyika katika Hospitali ya Zakhem, Dar es salaam.

DC Jokate kupitia kwa Mwakilishi wake Theodora ameishukuru pia Taasisi ya Hatua Group Afrika kwa kuwapatia vifaa vinavyotumika wakati wa kujifungua kwa kina Mama wapatao 200 na kutoa wito kwa kina Mama hao kuzingatia lishe bora pamoja na kufanya mazoezi hata baada ya kujifungua.

“Tunawashukuru sana na zawadi hizi tutaenda kuzitoa kwenu, tukiamini itakuwa ni motisha ya kuendelea kukumbuka kwamba tulifanya jambo hili siku fulani katika Hospitali hii ambayo itaturahisishia sisi tuwe tunakula vizuri lakini vilevile tuzingatie mazoezi na tuhudhurie kliniki.

Sabrina Shabani ni miongoni mwa Wanawake waliopata msaada huo ameishukuru Taasisi hiyo kwa kutoa msaada kwa kina Mama wajawazito pamoja na elimu waliyopatiwa kuhusu umuhimu wa lishe bora, mbio hizo za Temeke Martenal Jogging zenye kauli mbiu isemayo ‘Ujauzito wenye Afya, Utoto wenye Afya’ zinatarajia kuanza February mwaka 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live