Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate apongeza amani,  utulivu kwenye maonesho

C4bb358264254a63ea66c9785d3f161b.jpeg Jokate apongeza amani,  utulivu kwenye maonesho

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwengelo amesema wananchi wa wilaya hiyo wamefarijika kwa amani, utulivu na usalama uliokuwapo katika kipindi chote cha Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF).

Jokate aliyasema hayo kwa niaba ya wananchi wa Temeke wakati Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipozungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu tathimini na hafla ya kufunga maonesho hayo.

Alisema wana furaha na fahari kubwa kutokana na mafanikio yaliyofikiwa katika maonesho hayo ikiwako utulivu, amani na usalama uliotawala wakati wote.

“Sisi watu wa Temeke tumefarijika sana kwa utulivu. Temeke tuna furahi maonesho yamefanikiwa, asanteni wote mlioshiriki kuwezesha haya na tuendeleze hali hii ya utulivu na usalama wakati wote,” alisema.

Aliipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa namna ilivyobuni na kuweka mitaa maalum ikiwamo Mtaa wa Machinga na kueleza kuwa ana matumaini mwakani watashiriki Wamachinga wengi zaidi kwani serikali inawapenda na kuwathamini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka alimuhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa wana uhakika mwakani Wamachinga wengi watashiriki katika maonesho hayo na kuboresha mitaa waliyobuni mwaka huu ambayo ni ya madini, kilimo, wasanii na machinga.

Chanzo: www.habarileo.co.tz