Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate amtafakari Magufuli katika siku yake ya kuzaliwa

13325 Jokate+pic Jokate amtafakari Magufuli katika siku yake ya kuzaliwa

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amesema ameitumia siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa kwa kutafakari maisha na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Mwegelo ambaye kila Machi 20, huadhimisha siku yake ya kuzaliwa amesema siku hiyo alikuwa katika majonzi kutokana na kifo cha kiongozi huyo.

Amesema Magufuli ameongoza Taifa kwa kujitoa licha ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

“Ukaweka uhai wako rehani kwa ujasiri, uthubutu, ubunifu na upendo mkubwa wa dhati kwa wananchi na taifa letu tukufu Tanzania.”

“Kama sehemu ya vijana uliotuamini kwenye serikali yako, tutaendelea kuenzi mema yako yote kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Nitoe pole kwa mama yangu mama Janet Magufuli na watanzania wote,” amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz