Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate ‘Sikujiona Mkuu wa Wilaya, niliutamani Ubunge’

11366 Jokate+pic TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Jokate Mwegelo aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 nyuma ya Wema Sepetu, aliapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiahidi kuwatumikia wananchi wake, kulinda na kuitetea katiba ya nchi.

Amekabidhiwa mikoba kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Happness Seneda, baada ya kuingia ofisini kwa mara ya kwanza mwandishi wa Mwananchi, Rhobi Chacha alifanya naye mahojiano haya:

Mwananchi: Habari yako? Hongera sana kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Zipo habari kuwa ulikuwa kimya sababu ulikuwa unatengeneza nafasi ya ukuu wa Wilaya kwa ulikuwa ushajua, ni kweli?

Jokate: Hapana sikujua, kwanza watu waelewe huu uteuzi ulinishtua mimi na familia yangu, hakuna aliyekuwa anategemea hili suala na nilikaa kimya kwa ajili ya masuala binafsi na sio sababu ya kutengeneza nafasi ya ukuu wa wilaya, hiyo nakataa kuwa nafasi inakuja kwa ajili ya mtu akikaa kimya.

Kuhusu kimya kwenye mitandao, nilijitafakari nifanye mambo yangu binafsi kwenye maisha yangu, ndio maana nimepotea mitandaoni.

Mwananchi: Uliwahi kufikiri kama utakuwa Mkuu wa Wilaya?

Jokate: Sikuwahi kufikiri kama nitakuwa Mkuu wa wilaya ila nashukuru kwa hii heshima niliyopewa na Rais Magufuli kuniteua, kwani binafsi nilikuwa tu na ndoto ya kuwa kiongozi lakini sio ukuu wa wilaya.

Mwananchi: Katika Siasa, nafasi gani ulitamani kugombea?

Jokate: Nafasi niliyokuwa naitamani kwenye siasa ni kugombea ubunge, sikutegemea na wala sikuwa na wazo la ukuu wa wilaya.

Mwananchi: Kuna madai ya kuwa ulitumbuliwa UVCCM kwa kuwa ulipwaya nafasi hiyo?

Jokate: Hahaha sio kweli bwana, ningepwaya nisingekuwa nafasi hii hapa ya ukuu wa Wilaya.

Mwananchi: Watu wengi wanataka kujua, baada ya kuwa Mkuu wa Wilaya, je utaendelea na Uanamitindindo?

Jokate: Jamani mimi bado mrembo bwana.. hivyo sitaacha kuwa mwanamitindo sababu ya kuwa mkuu wa wilaya, kwani bado navaa na nitaendelea kuvaa kwani kuna nguo kama vitenge, suti na mavazi mengine yabuniwayo ambayo unaweza kwenda nayo sehemu yeyote.

Japo kwa sasa lazima kuwe na utaratibu wa mavazi lazima nibadilike kidogo, unakuja na utumishi wa umma, kuna mitindo mbalimbali mafuta, wanja ni urembo lazima tuendelee nao sababu ni maisha ya kila siku.

Na sio kama nitashiriki sana ila nitashiriki kama uwezo nitakuwa nao kuvaa mitindo inayobuniwa na wanamitindo mfano kama hii nguo niliyovaa imebuniwa na mwanamitindo wa Kitanzania nitaachaje urembo bwana, hivyo nitaendelea kusapoti mitindo mbali na huu huu ukuu wa wilaya wangu.

Mwananchi:Unawaahidi nini wananchi wa Kisarawe?

Jokate:Siwezi kutoa ahadi ila wasubiri vitendo vyangu, na cha msingi ni kushirikiana nao kupromoti shughuli zao mbalimbali za maendeleo.

Mwananchi: Vipi kuhusu masuala ya starehe utaendelea nayo?

Jokate: Unajua lazima tuheshimu mamlaka ya uteuzi kwani ni heshima ujue, hayo mambo mengine yatafuata.

Chanzo: mwananchi.co.tz