Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi wakala wa Kisbo Express alivyofariki kwa kukanyagwa na basi

100465 Pic+kisbo Jinsi wakala wa Kisbo Express alivyofariki kwa kukanyagwa na basi

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza/Shinyanga. Athmani Omari ambaye ni wakala ya mabasi ya kampuni ya Kisbo Express yanayofanya safari kati ya mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam amefariki dunia kwa kukanyagwa na tairi la nyuma la basi alilokuwa akilisindikiza.

Omari maarufu Mrangii anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 hadi 40 amefariki dunia leo Ijumaa Machi 27, 2020 katika tukio lililotokea stendi kuu ya mabasi mjini Shinyanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magirigimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulizungumzia zaidi baada ya kupata taarifa kutoka kwa maofisa wake waliokuwa eneo la tukio.

“Niko safarini Wilaya ya Kahama  lakini nimepokea taarifa hizo na nitazizungumzia zaidi nikifika mjini Shinyanga baada ya kupokea maelezo kutoka kwa wasaidizi wangu wanaolishughulikia suala hilo,” amesema Kamanda Magiligimba.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo, wakala mkuu wa mabasi hayo jijini Mwanza, Said Ramadhani amesema taarifa za kifo cha mwenzao zimewashtua kwa sababu wameachana naye leo alfajiri akisindikiza basi lililokuwa linaelekea jijini Dar es Salaam.

“Marehemu Athmani ameanza kazi ya kusindikiza mabasi wiki mbili tu zilizopita  nimeachana naye saa 12:00 asubuhi leo pale standi ya Nyabulogoya jijini Mwanza na alipaswa kuishia mjini Shinyanga,” amesema Said.

Pia Soma

Advertisement
Amesema wakati wa uhai wake, marehemu Athmani alikuwa anaishi eneo la Buhongwa jijini Mwanza na kwamba taratibu za msiba huo zitatangazwa baadaye baada ya mawasiliano na familia.

 Imeandikwa na Johari Shani (Mwanza) na Stella Ibengwe, Shinyanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz