Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi mradi wa umeme mto Rufiji utakavyookoa ukataji miti ovyo

68350 Pic+kelemani

Fri, 26 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Medard Kalemani amesema mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji utasaidia kutunza mazingira kwa maelezo kuwa asilimia 71.2 ya Watanzania wanatumia nishati ya kuni na mkaa kutokana na kukosa nishati mbadala ikiwemo umeme.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 26, 2019 kabla ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuweka jiwe la msingi katika mradi huo.

“Utasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira maana magunia ya mkaa milioni tano kila mwezi yanatumika na asilimia 71.2 ya Watanzania wanatumia nishati mbadala ya mkaa na kuni, Takribani ekari 800,000 hukatwa tukiendelea hivi kufikia mwaka 2030 takribani ekari 2.8 milioni zitakatwa kwa ajili ya kupata nishati ya mkaa na kuni,” amesema Kalemani.

Amesema mradi huo ni mkakati wa kupambana na mazingira na bila hivyo ingesababisha athari nyingi, na kwamba kazi muhimu katika mradi huo ni ujenzi wa bwawa kubwa litakaloweza kuhifadhi maji ya mita za ujazo 33.2 bilioni.

Ametaja faida nyingine kuwa ni kujengwa mashine tisa  zitakazozalisha megawati 235 kila moja na hivyo kufanya jumla ya megawati 2,115.

“Tutazalisha kilovoti 400 ni umeme mkubwa utakaowezesha kuzalisha umeme wa kutumika viwandani utakaosafirishwa kwenda Chalinze mpaka Dar es Salaam na mwingine mpaka Dodoma na ndiyo umeme utakaotumika pia katika treni ya mwendokasi.”

Habari zinazohusiana na hii

“Rais Magufuli ulitoa maelekezo kwamba lazima tupate megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 mradi huu ni kichocheo kikubwa sana kuelekea kupata megawati hizo utatosha sana kuendesha shughuli za viwanda,” amesema Kalemani.

Chanzo: mwananchi.co.tz