Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiko la mkaa lakatisha maisha ya watoto wawili

Jiko Pc Jiko la mkaa lakatisha maisha ya watoto wawili

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili wamefariki mkoani Iringa na mmoja amenusurika baada ya kujifungia ndani wakipika ugali kwa kutumia jiko la mkaa.

Watoto waliofariki dunia usiku wa kuamkia leo, Januari 22, 2024 ni Evance Kapinga (3) na Tabia Ngonile (17) huku Moline Mligo (7) akinusurika kwenye ajali hiyo, katika Mtaa wa Frelimo.

Hili ni tukio la pili kwa jiko la mkaa kukatisha uhai, ambapo mwaka jana mwishoni, mamalishe na mteja wake walikutwa wamefariki dunia ndani ya mgahawa katika eneo la Mkwawa, Manispaa ya Iringa baada ya kukoka mkaa kwenye jiko na kubandika maharage.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takribani watu milioni nne, hupoteza maisha kutokana na kupikia nishati ngumu ukiwemo mkaa na kuni.

Akisimulia tukio la watoto wawili kufariki dunia, jirani wa familia hiyo Ibrahim Kitang’ala amesema usiku wa manane aliamshwa na wazazi wa watoto hao waliorejea nyumbani na kugonga mlango bila mafanikio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live