Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiji wapongezwa kupeleka ‘kijani’ mitaani

A58a41e4049e966bbe68ba5dab6890d5 Jiji wapongezwa kupeleka ‘kijani’ mitaani

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameupongeza uongozi wa jiji la Dodoma kwa kusogeza kampeni ya kijanisha kwenye mitaa.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa zoezi la kupanda miti katila mtaa wa Miganga Kata ya Mkonze.

Dk Mahenge Dk Mahenge aliwapongeza pia wananchi wa Miganga kwa kuchimba mashimo ya kupanda miti zaidi ya 2,000 pembeni ya barabara na daraja la Dhambi.

Aliwataka wananchi hao kuendelea kutunza miti hiyo ambayo itasaidia kuifanya Dodoma ya Kijani kama miti hiyo itapona.

Aliitaka mitaa mingine 221 ya Jiji la Dodoma kuiga mfano wa Miganga kuchimba mashimo na kupanda miti kwa ajili ya Kukijanisha Dodoma lakini pia kupata vivuli na matunda.

Aliiagiza Walala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanaboresha barabara za mitaa pamoja na kurekebisha daraja la Dhambi ili liwe la amani na upendo.

Pia Dk Mahenge aliliagiza Jiji kukaa na viongozi wa mtaa huo kumaliza matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa eneo hilo.

Mkurugenzi aa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru aliwataka wananchi wa maeneo husika kushirikiana na madau wa mazingira wa jiji.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga, Ludovick Choga alipongeza uamuzi wa mkuu wa mkoa kushiriki kupanda miti mtaani hapo na kupatya nafasi ya kusiklia changamoto mbalimbali za mtaa huo.

Ofisa Mazingira wa Jjii, Dickson Kimaro aliwataka wananchi wa Miganga kutunza miti hiyo.

Aidha alisema kampeni ya kupanda miti ni endelevu na watendaji wa Jiji kila Jumamosi watakuwa wakigawanyika kwenda mitaani, kwenye taasisi na vyuoni kushiriki katika kampeni ya Kuikijanisha Dodoma hadi mwisho wa msimu wa mvua.

Chanzo: habarileo.co.tz