Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiji latenga bil1/- kwa maji, barabara

87f97ae72c2a2dfbb283c3d3a7fc7096.jpeg Jiji latenga bil1/- kwa maji, barabara

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetenga Sh bilioni moja ili kuimarisha miundombinu ya barabara na upatikanaji wa maji.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alibainisha hayo ya mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea, kujadili na kupitisha Bajeti ya Mwaka 2020/2021.

Alisema hatua ya kutenga fedha hizo ni ipo katika mkakati wa kuendelea kustawisha Jiji la Dodoma.

"Tunajua kuna mamlaka zinazoshughulika na maji na barabara, lakini tukaona tutenge fedha hizo kutoka mapato ya ndani Ili upatikanaji maji uimarike na pia Tarura (Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini) waweze kuimarisha barabara zetu na kuboresha mitaro ya maji ili ziwe za kupitika, lakini pia tufikishe kwenye maeneo mapya," alisema.

Kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, halmashauri imepanga bajeti ya Sh bilioni 120.8 na asilimia 83 ya fedha hizo zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika nusu mwaka ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2020/2021, Mafuru alisema ni pamoja na kwa halmashauri kukusanya Sh bilioni 14.76 za mapato ya ndani zilizoelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, fidia na kuimarisha huduma za kijamii za afya na elimu.

Alisema pia Halmashauri ya Jiji la Dodoma limefanikiwa kutoa leseni 15,512 za biashara huku ikitumia takribani Sh bilioni 11.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kimkakati wa kujenga hoteli na ujenzi wa mradi wa kumbi na hoteli unaojengwa Mji wa Serikali.

"Mradi wa ujenzi wa hoteli inayojengwa katikati ya Jiji umefikia asilimia 90 na inatarajia kuanza Aprili mwaka huu huku mradi wa Mji wa Serikali ujenzi wake umefikia asilimia 60.

Alisema kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa miradi hiyo kutalifanya jiji kuongeza mapato ya ndani ambapo hoteli inatarajia kuingiza Sh bilioni moja kwa mwaka na Mji wa Serikali unatarajia kuingiza takribani Sh milioni 800 kwa mwaka.

Aidha, Mafuru alisema mafanikio mengine ni kustawisha Jiji la Dodoma ambapo Sh bilioni 1.3 zimetumika katika kuthamini, kusanifu na kulipa fidia kwa maeneo kadhaa ya jijini hapa.

Alisema katika nusu ya mwaka 2020/2021, viwanja 59,139 vimepimwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz