Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiji la Arusha ladai bil 3/- makundi maalumu

334941025570752ddfeadfd15e3fa288 Jiji la Arusha ladai bil 3/- makundi maalumu

Fri, 16 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JIJI la Arusha linawadai Sh bilioni tatu wanawake, vijana na wenye ulemavu waliochukua mkopo wa asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri.

Akizungumza jana katika utoaji mikopo kwa vikundi 42 katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021, Ofisa Tarafa ya Elerai, Tito Cholobi, alisema jiji linadai fedha hizo kwa makundi hayo maalumu baada ya wadaiwa wengine kushindwa kurejesha na wengine kutokomea kusikojulikana.

Alisema fedha zinazodaiwa zinatokana na mikopo hiyo iliyotolewa katika kipindi cha miaka mitatu huku baadhi ya wanufaika wakikosa uaminifu kiasi na kisha wanapopewa mikopo huzima simu na wengine kuhama mitaa.

"Jamani fedha hizi ni za serikali, mkizichukua rudisheni na wenzenu wengine wakope acheni tabia mbaya ya kutorejesha mikopo, oneni licha ya kuwadai Sh bilioni tatu, bado tunaendelea kutoa mikopo mengine hamjiulizi fedha hizi zinatoka wapi,"alihoji.

Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha, Mwanamsiu Dossi alisema kati ya Julai hadi Desemba, Halmashauri ya Jiji la Arusha imeidhinisha utoaji wa mikopo ya Sh 565,380,410 kwa vikundi 42 vya wajasiriamali vilivyopo kata 23 jijini humo.

Alisema fedha hizo zinakopeshwa kutokana na mchango wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ambapo Sh milioni 35 zitatolewa kwa vikundi 25 vya wanawake na Sh milioni 175 zitatolewa kwa vikundi 15 vya vijana na Sh milioni 30 zinatolewa kwa vikundi viwili vya watu wenye ulemavu.

Ofisa Vijana Jiji la Arusha, Hanifa Ramadhan alisema jiji hilo litaendelea kushirikiana na vijana kuibua miradi mbalimbali na mikopo ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Aliwasisitiza vijana wanapopata mikopo kuitumia kwa uangalifu na kurejesha marejesho ili kuwezesha na wengine kukopa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz