Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la polisi Songwe lagawa taulo za kike

Jeshi La Polisi Songwe Lagawa Taulo Za Kike Jeshi la polisi Songwe lagawa taulo za kike

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe limegawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule msingi Izuba pamoja na vifaa vingine vitakavyowasaidia kwenye masomo yao.

Wakikabidhi vifaa hivyo tarehe 24 Oktoba 2023 kupitia Mtandao wa Polisi wanawake TPF Net mkoa wa Songwe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Veronica Myovela pia walitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi hao kuhusiana na madhara ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Aidha, wanafunzi hao wameaswa kutojihusisha ama kujiingiza kwenye vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ambavyo vinaweza kuharibu ndoto zao za baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live