Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo lateketea kwa moto Mwanza- Video

Moto Moto Mwanza (600 X 334) Jengo lateketea kwa moto Mwanza

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Habarileo

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umezuka na kuteketeza jengo la ghorofa moja linalotumiwa na wafanyabiashara katika Mtaa wa Rwagasore katikati ya Jiji la Mwanza.

Katika jengo hilo ambalo liko umbali usiozidi Kilometa moja kutoka zilipo Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Mwanza kuna maduka ya wafanyabiashara wa vifaa kieletroniki na vyombo vya muziki.

Mashuhuda wanasema moto huo umeanza Saa 6:00 mchana ambapo baada ya kuibuka wamiliki wanadai kuwa umeibuka kutokea eneo la juu la jengo hilo lenye ghorofa moja. Bado Maofisa wa Zimamoto na Uokoaji wanaendelea na jitihada za kudhibiti moto huo usisambae katika majengo mengine.

View this post on Instagram

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)



Taarifa zaidi zinakujia hivi punde
Chanzo: Habarileo