Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo laporomoka na kuua wanne, huku 17 wakijeruhiwa (+Video)

Goba Jengo Jengo la Ghorofa laporomoka na kuua wanne

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa, baada ya jengo la ghorofa ambalo lilikuwa linajengwa kuporomoka na kuangukia nyumba za majirani katika eneo la Goba kwa Awadhi, Dar es Salaam .

Tukio hilo limetokea leo Disemba 6. Akizungumza kutokea eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya ubungo, Kheri James amesema;

"Jengo lilikuwa linajengwa limeanguka, katika ajali hii majeruhi wapo 17, pia tunazo maiti 4 (Wanaume wawili na Wanawake wawili), Wanaume wawili ni Mafundi waliokuwa wanajenga na Wanawake wawili ni Wakazi wa nyumba za Jirani zilizoangukiwa na Jengo"

Juhudi za uokoaji zinaendelea katika eneo hilo.

Tanzama Video hapa Chini, kuona uharibifu mkubwa ambao umetokea

Chanzo: www.tanzaniaweb.live