Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la uchunguzi daraja la kwanza kujengwa Arusha

F8e7db674cf5433d6e5cf2eb2d371e58 Jengo la uchunguzi daraja la kwanza kujengwa Arusha

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, ameahidi kujenga jengo la uchunguzi daraja la kwanza jijini Arusha atakapochaguliwa tena kuwa rais.

Alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wake wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Shehe Amri Abeid jijini humo.

Aidha aliahidi kuendeleza sekta ya afya kwa kujenga zahanati na vituo vya afya na kusambaza vifaa tiba na wahudumu wa afya. Alisema pia ataendelea kutoa elimu bure na kuboresha miundombinu na kujenga shule moja ya wasichana katika kila mkoa na kupeleka vifaa vya tehama.

Magufuli alisema mji wa Arusha ni mji wa kitalii, hivyo ataendeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 520 ili kutosheleza wakazi wa Arusha na nyongeza itasambazwa kwa wananchi wa wilaya za Hai na Simanjiro.

Aliwaombea kura wagombea ubunge na udiwani wa CCM. Alisema aliwateua kwa kuwa anawajua ni wachapakazi na wanajali maslahi ya wananchi. Pia aliwapongeza wananchi wa Arusha kwa kuendelea kutunza mazingira ya kijani hadi leo kama yalivyokuwa mwaka 1984 alipofika Arusha kwa mara ya kwanza alipokwenda kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Makuyuni.

Alisema anataka Arusha iwe ndiyo Calfornia ya Tanzania, jambo ambalo atalifanya endapo watampa ridhaa ya kuongoza kwa miaka mingine mitano ijayo. Aliwataka waendelee kuitunza amani, kwa kuwa palipo na amani ndiyo penye maendeleo.

Akuzungumzia sekta ya utalii, alisema inaingiza pesa nyingi, hivyo ataimarisha usafiri wa anga kwa kununua ndege nyininge tano moja ikiwa ni ya mizigo. Pia alisema ataweka mabehewa ya treni yenye huduma ya ubaridi ili mboga na matunda viweze kusafirishwa kwa usalama. Aliahidi pia kujenga jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).

Chanzo: habarileo.co.tz