Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la kihistoria Iringa

Iringa Boma Museum Jengo la kihistoria Iringa

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Iringa Boma, Jimson Sanga amewashauri Wananchi mkoani Iringa na mikoa jirani kuwa na desturi ya kufanya utalii katika kituo cha Boma ambalo ni jengo la historia la kijerumani.

Sanga ameyasema hayo akiwa katika kituo hicho ikiwa ni mwendelezo wa ziara zinazofanyika kuelekea kilele cha karibu kusini Septemba 27, 2023 yaliyoanza Septemba 23, 2023.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa jengo la Boma ni moja ya kituo cha utalii kilichotumika kama zahanati ya kuwatibu wakoloni wa Kijerumani ambacho mpaka sasa bado jengo hilo linatumika kufanya shughuli mbalimbali za kiutalii ikiwa ni pamoja na kupata masimulizi ya historia ya mkoa wa Iringa.

“Jengo hili waliofanya ujenzi kwa miaka hiyo ni wenyeji ambao ni Wazee wa mji wa Iringa,” amesema Sanga.

Ikumbukwe mikoa takribani 10 inayounganisha kusini nzima unaendelea kusherekea utalii wakusini unaofanyika katika viwanja vya kihesa kilolo mkoani Iringa na kilele Cha maeonesho hayo ikiwa ni tarehe 27/9/2023 ambapo yatahimishwa ramsi mpaka mwakani.

Huku lengo la maonesho haya ikiwa ni kuhakikisha utalii wa kusini unatangazwa na kuwafikia watu wengi zaidi duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live