Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la NSSF Tanga lanusurika kuteketea kwa moto

NSSF Jengo Jengo la NSSF Tanga lanusurika kuteketea kwa moto

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga limenusurika kuteketea kwa ajali ya Moto uliotokea alfajiri ya leo, moto ulioanzia kwenye ofisi ya Mhasibu na kuteketeza baadhi ya vitu vilivyopo katika ofisi hiyo kabla ya kudhibitiwa na Jeshi la Zimamoto mkoa wa Tanga huku Majeruhi akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Bombo

Akizungumza mara baada ya Kudhibiti moto huo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Tanga, Mrakibu Abrahaman Ntezidiyo amesema wamefanikiwa kuudhibiti moto kabla ya kuleta madhara kwenye ofisi nyingine huku chanzo cha moto huo bado hakijajulikana

Kwa Upande wake Meneja mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa Nuhu Mmbaga amelishukuru jeshi la Zimamoto mkoa wa Tanga kwa kuweza kudhibiti moto katika Ofisi ya jengo hilo, ambapo pia amewahimiza wananchi kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapotokea ili kuweza kudhibitiwa mapema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live