Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamii yatakiwa kuwasaidia wenye ulemavu

79813 Ulemav+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Uongozi wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Amani Center kimewaomba watu wa kada mbalimbali na taasisi za Serikali  kuwakatia bima ya afya watoto hao wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Ombi hili limetolewa na Ofisa ustawi wa jamii ambaye pia ni mtendaji mkuu wa kituo hicho,  Salvatory Agustino wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta duniani.

Katika siku hiyo uongozi wa shirika hilo Mkoa wa Morogoro walitoa msaada wa mchele, maharage, unga, sabuni, mafuta ya kupikia.

Amebainisha kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma za afya kwa kuwa watoto wengi wameshavuka umri wa kutibiwa bure.

Meneja wa shirika la Posta mkoa wa Morogoro,  Magreth Mlyomi amesema katika kuadhimisha siku ya Posta duniani, shirika hilo limeshiriki kutoa msaada kwa watoto wenye ulemavu wanaoishi katika kituo hicho.

Ameitaka jamii kuacha kuwatenga watoto wenye ulemavu badala yake wawapatie haki zao kama wanavyopewa watoto wengine.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz