Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa ajiua kisa kufumaniwa na mwanafunzi wa kidato cha kwanza

Mauaji Abc.jpeg Jamaa ajiua kisa kufumaniwa na mwanafunzi wa kidato cha kwanza

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

John Mhagama (42) Mkazi wa Mtaa wa Kanisa B, Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe amejiua kwa kunywa sumu baada ya kufumaniwa na mke wake akiwa kwenye mazungumzo ya kimapenzi na mwanafunzi wa Kidato cha kwanza anayeishi maeneo ya jirani na nyumbani kwao.

Imeelezwa kuwa kila jioni, Mhagama alikuwa akiaga anakwenda kununua mkaa wa matumizi ya nyumbani kisha akawa anakutana na mwanafunzi huyo na kumpa pesa.

Siku ya tukio Mhagama alienda kununua mkaa kama kawaida yake lakini siku hiyo mkewe alikuwa akimfuatilia kwa nyuma na kumuona mumewe akiongea na mwanafunzi huyo na kumpa Tsh. 5,000 huku akimbembeleza kumkubalia ombi lake la kuwa wapenzi kwani amekuwa akichukua pesa zake pasipo kumtimizia hitaji lake.

Mkewe alijitokeza na kuanza kumlaumu mumewe kwa kitendo alichofanya lakini kwa hasira Mhagama alimpiga mkewe na kisha kurudi zake nyumbani ambako alikunywa sumu na kufariki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuitaka Jamii kutokuwa na wivu uliopitiliza kwakuwa mara nyingi matokeo yake huwa mabaya na kupelekea vifo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live