Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jakuzi la sh milioni 6.5 kwenye nyumba ya DED lazua gumzo

Jakuzi A0001 Jakuzi la sh milioni 6.5 kwenye nyumba ya DED lazua gumzo

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Kigoma wamehoji uhalali wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma kiasi cha Sh milioni 6.5 kuweka Jakuzi la kuogea kwenye nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo wakati halmashauri inachangamoto kubwa ya fedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Hali hiyo imetokea wakati wajumbe hao waliokuwa na kikao cha kawaida cha jumuiya hiyo kwa Mkoa wa Kigoma walipotembelea kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ya halmashauri hiyo ikiwemo nyumba hiyo ya mkurugenzi mtendaji.

Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kigoma, Jacskon Mateso aliuliza watendaji wa halmashauri hiyo waliokuwa wakiongoza ziara hiyo kwamba halmashauri ilizingatia nini kuweka Jakuzi hilo kwa bei hiyo wakati bado halmashauri inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi.

Wakiwa katika eneo hilo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Exavery Ntambala alitoa taarifa kuwa nyumba hiyo ya Mkurugenzi na nyumba nyingine ya watumishi iliyopo kwenye eneo hilo zimejengwa kwa gharama ya Sh milioni 270 na jakuzi kwenye nyumba ya mkurugenzi imegharimu zaidi ya Sh milioni sita.

Diwani wa viti maalum Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Asha Omari alisema kuwa hayo ni matumizi mabaya ya fedha za serikali wakati halmashauri ina mzigo mkubwa wa kugharamia miradi mbalimbali ya wananchi huku fedha nyingi zinatumika kujenga kitu kimoja cha anasa bila sababu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live