Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji mstaafu Warioba akagua miradi ya SUA

Warioba Pc Data Jaji mstaafu Warioba akagua miradi ya SUA

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Jiji mstaafu Joseph Warioba amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na chuo hicho ikiwa ni miaka mitano ya uongozi wake tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa chuo hicho.

Baadhi ya miradi aliyetembelea Jiji mstaafu Warioba ni pamoja na mradi wa ujenzi wa maabara mtambuka, hospitali ya rufaa ya mifugo na mradi mabwawa ya kutotorishea vifaranga vya samaki.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Raphael Chibunda ziara ya mkuu wa chuo imelenga kuangalia kuangalia utekelelezaji wa miradi hiyo na kwamba ziara hiyo utaendelea Oktoba 26 kwa kutembelea mradi wa kutengeneza samani uliopo kwenye kampasi ya Solomoni Mahrangu.

Awali akizungumza na vijana wanaofundishwa kilimo biashara cha mbogamboga na matunda kwa kutumia kitalu nyumba kwa ushirikiano wa Sua na Pass Jiji walioba alikitaka chuo hicho kuandaa maeneo ili vijana hao waweze kuendelea na shughuli hiyo mara baada ya kufuzu ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Jaji mstaafu Warioba alisema kwa mujibu wa takwimu kwa sasa nchi inakadiliwa kuwa na watanzania 60 milioni na baada ya miaka 40 kutakuwa na ongezeko la watu linalokadiliwa kuufikia 100 milioni hivyo lazima kama nchi iwe na utosherezi wa chakula.

"Kutokana na ongezeko la idadi ya watu Sua inabidi wawaandae vijana hawa ili waweze kufanya kilimo biashara na sio waishie kujifunza tu," amesema Jiji mstaafu Warioba.

Chanzo: mwananchidigital