Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji mstaafu Rugazia kuzikwa Ijumaa kijijini kwake Rwamashonga

70279 Pic+kuzikwa

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa Jaji Mkuu mstaafu wa nchini Tanzania, Projest Rugazia utazikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 katika Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

Jaji Rugazia alifariki dunia alfajiri ya kuamkia Jumapili Agosti 4, 2019 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shughuli za mazishi, Charles Gabikwa alisema saa 6.30 mchana mwili wa Jaji Rugazia utatolewa nyumbani kwake Kinondoni kuelekea Kanisa Katoliki la Mtkatifu Peter lililopo Oysterbay.

Gabikwa alisema Ibada itaanza  Saa 7 mchana hadi saa 9 mchana na kuanzia saa 9:05 hadi saa 10, zitatolewa salamu za rambirambi.

“Watu watatoa heshima zao za mwisho kanisani baada ya hapo, mwili wa marehemu Jaji Rugazia utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) na kesho Alhamisi Agosti 8, 2019 utasafirishwa kuelekea kijijini kwao Rwamashonga, Wilayani Missenyi mkoani Kagera.

Amesema Ijumaa Agosti 9, 2019  wakazi wa eneo hilo watatoa heshima zao za mwisho na baadaye mwili wake utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Pia Soma

Jaji Rugazia alizaliwa Agosti 28, 1954 mkoani Kagera, alianza kazi rasmi Januari 01, 1983 kama Hakimu Mkazi.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Machi 28, 2003 na  alistaafu rasmi Agosti 28, 2016 akitokea Mahakama Kuu - Divisheni ya Ardhi.

Chanzo: mwananchi.co.tz