Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mohamed Chande Othman kufungua mkutano wa kimataifa Arusha

28977 Jaji+pic TanzaniaWeb

Tue, 27 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania,Mohamed Chande Othman anatarajiwa kufungua mkutano wa siku nne wa wataalamu wa sheria kutoka mataifa mbalimbali duniani ili kuweka mikakati ya kukabiliana na uhalifu wa makosa ya jinai wa kimataifa .

Mkutano huo unaoanza  Jumatatu utafunguliwa na Jaji Chande aiku ya   Jumanne  na utafanya tathmini ya mpango wa miaka miwili ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sheria wakiwamo majaji na waendesha mashtaka katika nchi za Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika waTtaasisi ya Wayamo Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Afrika la Haki na Uwajikaji(AGJA) yenye makao yake Kenya, Joseph Roberts Mensah , mkutano utatoa fursa muhimu kwa wataalamu hao.

 “Uwepo wa wataalamu hawa utatoa fursa ya kujadiliana na kuzipatia majibu sahihi changamoto na kuona uhusiano kati ya uhalifu wa unaovuka mipaka na uhalifu wa kimataifa, pia ongezeko la uhalifu unaovuka mipaka na wajibu wa taasisi za kisheria katika ngazi za kanda na nchi husika kukabiliana na uhalifu,”anaeleza taarifa.

 Viongozi wengine watakaohudhuria ni pamoja na mkurugenzi wa mashtaka nchini,Biswalo Mganga,jmwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda,Jean –Bosco Mutangana, mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini, Robert Boaz pamoja na mkurugenzi mkuu wa Wayamo Foundation,Bettina Ambach.

Mkutano huo utahudhuriwa pia na mpelelezi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Jinai,The Hague nchini Uholanzi,William Rosato na kuwa waendesha mashtaka na wakuu wa idara za upelelezi wa makosa ya jinai kutoka Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda watakuwa na mkutano wao wa kubadilisha uzoefu.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz