Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mkuu ataka wahitimu IJA kuitumia Tehama

A846e900d7eb2b21da31715a24c4f4c5 Jaji Mkuu ataka wahitimu IJA kuitumia Tehama

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameutaka uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kuhakikisha wahitimu wanaomaliza chuoni hapo wanamudu matumizi ya Tehama pamoja na kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuingia katika kazi ya ushindani.

Alisema hayo katika mahafali ya 20 chuoni hapo yakiwa yameambatana na maadhimisho ya kilele cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Profesa Juma alisema wanafunzi wanaotokana na chuo hicho lazima wawe wanafunzi wa karne ya 21 na karne ya 21 inaongozwa na wanawake tofauti na karne zilizopita zilikuwa zikiongozwa na wanaume na kuwataka wajaribu kuwapandisha wanafunzi wa astashahada na stashahada ili wawe sambamba na mapinduzi makubwa yanayoendelea katika matumizi ya tehama katika huduma mbalimbali.

“Wahitimu wenu lazima wafahamu namna kanuni za ufunguaji wa mashauri kwa njia ya eletroniki zinazotumika kila siku mahakamani ili wawe wanafahamu namna gani tehama inatumika mahakamani,” alisisitiza Profesa Juma.

Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo, Dk Gerald Ndika alisema tafiti mbalimbali za wataalamu wa uchumi duniani zinaonesha kuwa nchi ambazo uchumi wake umekuwa kwa kiasi ni nchi ambazo zimewekeza zaidi kwenye maarifa na ujuzi.

Alisema chuo kimeendea kufanya vizuri katika teknolojia ya habari ya mawasiliano kwa kuakisi hilo chuo kimeendelea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kimataifa ikiwemo taasisi ya mafunzo na utafiti ya umoja wa mataifa (United Nations Institute for Trainning and Research –UNITAR) iliyopo Uswisi.

Dk Ndika alieeleza kuwa zimekuwepo juhudi zinazofanywa na uongozi wa chuo katika kukarabati majengo yaliyopo ili kukidhi mahitaji na nyezo za ufundishaji na huduma bora kwa wanachuo na wafanyakazi.

Mkuu wa chuo hicho, Dk Paul Kihwelo alisema licha ya mafanikio yaliyopo chuoni hapo katika ngazi ya stashahada na astashahada chuo kimeendelea kutekeleza kwa vitendo malengo ya kuanzishwa kwake kwa kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa mahakama ngazi mbalimbali ikiwemo majaji wa mahakama kuu na mahakama ya rufani lakini pia mahakimu wapya.

Dk Kihwelo alibainisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni chuo kimejiimarisha kutoa ushauri pamoja na utafiti na pia sasa chuo kina miradi kadhaa.

Chanzo: habarileo.co.tz