Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo ampa Ded siku 30

88765 Jafo+pic Jafo ampa Ded siku 30

Tue, 17 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Momba: Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya Momba, Adriano Jungu kujitafakari juu ya utendaji wake ili kuiweka halmashauri yake vizuri.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo muda mfupi uliopita mjini Chitete makao makuu ya wilaya ya Momba wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo kuwa mkurugenzi huyo ameshindwa kuisimamia halmashauri, matokeo yake hakuna ufanisi unaopatikana kwenye usimamizi wa miradi.

Ametaja baadhi ya mapungufu ya mkurugenzi huyo kuwa ni pamoja na kushindwa kusimamia miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa soko la kimataifa la mazao, kushindwa kukusanya mapato ya ndani na kushindwa kuwaunganisha watumishi ili wafanye kazi kama timu moja.

"Nakuagiza mkurugenzi ujitathmini mwenyewe ndani ya siku 30 kama viatu ulivyopewa vinakutosha na pia nataka uanze kwa kuhakikisha soko la mazao linakamilika na ifikapo Januari 15, 2020, unipigie picha wewe mwenyewe na unitumie kupitia WhatsApp," amesema Jafo.

Jafo amemuagiza mkuu wa mkoa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela kuwa karibu na halmashauri hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz