Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JINAI: Watoto walawitiana kulipa kisasi Tabora

JINAI: Watoto walawitiana kulipa kisasi Tabora

Tue, 7 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Idadi ya watoto wa kiume wenye umri wa kati ya miaka ya 14 na 17 wanaojitumbukiza katika vitendo vya ulawiti imeongezeka mkoani Tabora.

Watoto hao wanapofikishwa katika vyombo vya sheria hubainika kujihusisha katika uharifu huo kwa sababu ya kulipa kisasi.

Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Tabora, Nehemia Steven alisema katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2019 walipokea mashauri 17 ya watoto ambako zaidi ya asilimia 60 yalihusu vitendo vya ulawiti.

“Mashauri 10 kati ya 17 yalikuwa ya ulawiti ambako yaliyohusisha watoto wenyewe.”

Alitaja mashauri mengine ni ya makosa ya kuua bila kukusudia na wizi.

“Hili tatizo la watoto kulawitiana ni kubwa na uchunguzi unaonyesha wengi wamekuwa wakilipiza kisasi kwa kuwa na wao walifanyiwa unyama huo,” alisema Steven.

Pia Soma

Advertisement
Ofisa huyo ambaye anahusika na mashauri ya watoto alisema uchunguzi umebaini watoto wanaotenda makosa hayo ni wanaolelewa na mzazi mmoja.

Alisema watoto wengine ni wale waliolelewa na wazazi walio katika migogoro ya kimahusiano.

Ofisa huyo alisema jamii inapaswa kuchukulia kwa uzito suala la malezi kwa watoto ili kuepuka vitendo vya kulipiza kisasi.

Awali makamu mwenyekiti wa Chama cha mawakili Tanganyika (TLS) kanda ya Tabora, Kanani Chombala alisema vitendo hivyo vinasababisha kuwa na Taifa lenye watoto watenda makosa.

Chombala aliwataka wazazi kuchua jukumu lao la malezi kwa lengo la kuwalinda watoto ili wasitumbukie katika mikono ya vyombo vya dola na kuharibu kabisa ndoto zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz