Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JESHI LA POLISI MKOA WA KASKAZINI LATOA WITO KWA WAMILIKI WA MAHOTELI

Maxresdefault 5?fit=1200%2C675 JESHI LA POLISI MKOA WA KASKAZINI LATOA WITO KWA WAMILIKI WA MAHOTE

Mon, 21 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja wamewataka wawekezaji wa mahoteli  kuhakikisha wanaweka Vifaa  vya kuzimia moto ili kuweza kuwa rahisi pindi pale panapotokea tatizo.

Akizungumza mara baada ya kutokea kwa moto kwenye hoteli Kamanda wa polisi wa mkoa huo Haji Abdallah Haji amesema tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 19-09-2020 majira ya 8:30 Usiku huko Kiwengwa Wilaya ya Kaskazin B Unguja.

Ameongeza kusema kuwa kumeungua hoteli Vera na kusababisha hasara kubwa na moto huo kuingia katika hoteli ya Blue Bay na kuuguza nyumba ya wafanyakazi na hakuna aliejeruhiwa katika tukio hilo na hadi sasa thamani haijajulikana na chanzo chake inasaidikiwa hitilafu ya umeme.

Nae Sheha Shehia ya Kiwengwa Maulidi Masoud Ame amekiri kupokea tukio hilo na kuwataka wamiliki wa mahoteli kuwa  na vifaa maalum vya kuzimia moto ingawa hoteli ya Blue Bay walikuwa navyo ikiwa rahisi kuzima moto lakini hoteli ya Vera hawakuwa navyo vifaa vya moto na kusababisha hasara kubwa.

Story na Rauhiya Mussa Shaaban 

Chanzo: zanzibar24.co.tz