Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iringa yatajwa kuongoza kwa udumavu Tanzania

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkoa wa Iringa umetajwa kuwa na asilimia 42 ya udumavu ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuliko wastani wa udumavu kitaifa ambapo ni asilimia 34.

Hata hivyo wakati Iringa ikiongoza kwa tatizo la udumavu, imeelezwa kuwa asilimia 10 ya Watanzania wana lishe iliyopitiliza kutokana na kula vyakula ambavyo havina mchanganyiko mzuri.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Dk Faustin Ndugulile ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatatu Aprili 15,2019 wakati akijibu swali la mbunge wa Kalenga (CCM) Godfrey Mgimwa ambaye amehoji ni vigezo gani vinatumika kufikia kwenye takwimu kuwa Iringa inaongoza kwa udumavu na akataka kujua hatua gani zitakazochukuliwa.

Dk Ndugulile amesema vigezo vilivyotumika kuangalia takwimu hizo ni kuchukua sampuli za kaya zilizochaguliwa kushiriki kupitia utaratibu maalumu wa kitaalamu

"Kwa kaya zilizochaguliwa, watoto wa chini ya umri wa miaka mitano walipimwa urefu, kimo, uzito, kupimwa wekundu wa damu pamoja na kuhoji maswali kwa mkuu wa kaya au mlezi wa kaya kwa kutumia dodoso maalum," amesema Dk Ndugulile.

Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kunusuru tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa na kutekeleza mpango mkakati jumuishi wa kitaifa wa utekelezaji wa afua za lishe.

Related Content



Chanzo: mwananchi.co.tz