Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iringa waanika mpango wa kuboresha huduma ya maji safi

C550479cd1610f8e21ad3e3a60be7d7d Iringa waanika mpango wa kuboresha huduma ya maji safi

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA) imeanika mpango wake wa biashara wa miaka mitatu, 2021/24 unaolenga kuboresha huduma ya majisafi kutoka asilimia 90 ya sasa hadi asilimia 98 na upatikanaji wa huduma kutoka saa 20 hadi saa 24 kwa siku.

Akitoa taarifa katika mkutano wa wadau wa mamlaka hiyo jana, Mkurugenzi wa IRUWASA, Gilbert Kayanga alisema mpango huo unahusisha kupanua mtandao wa maji kwa kulaza kilometa 120 za bomba za maji Iringa mjini na maeneo ya pembezoni ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Mpango huo unalenga pia kupanua mtandao wa maji katika miji ya Ilula na Kilolo, wilayani Kilolo, kubadilisha bomba chakavu na kufunga pampu mpya, kukarabati matangi na kujenga mengine sita mapya, kurekebisha maunganisho ya wateja na kuboresha na kulinda vyanzo vya maji.

Katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi, Kayanga alisema mamlaka hiyo itawasajili wateja wake wote katika mfumo wa kisasa wa GIS ili kurahisisha utoaji wa huduma.

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi aliipongeza mamlaka hiyo akisema ufanisi wake wa kazi umesababisha iaminiwe na kufanya kazi hadi nje ya mipaka ya manispaa ya Iringa.

Alisema utendaji mzuri wa IRUWASA umetambuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA) kwa kuitaja IRUWASA mwaka 2018 na 2019 kuwa Mamlaka ya pili kitaifa kwa kutoa huduma ya maji safi kwa viwango vinavyokubalika na mwaka 2018 kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa kutoa huduma ya usafi wa mazingira.

Alitaja maeneo yanapata huduma ya IRUWASA nje ya manispaa ya Iringa kuwa ni pamoja na kata za Kata za Luhota, Mseke, Kalenga, Kiwele, Kisinga na Kihorogota kwa Iringa Vijijini na Kilolo na Ilula kwa wilaya ya Kilolo.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa aliwaonya baadhi ya watu wanaohujumu miundombinu ya maji ya mamlaka hiyo kwa matumizi yao binafsi na kwamba serikali haitasita kuwashughulikia pindi watakapobainika.

Chanzo: habarileo.co.tz