Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iringa: Wananchi wafunga barabara

Kitwi Wakazi wa eneo hilo wamekua wakitilia hofu usalama wa watoto waendapo na kurudi shule

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa eneo la Kitwiru mkoani Iringa wamelazimika kufunga barabara kwa muda, wakishinikiza kuwekwa kwa alama ya wavuka kwa miguu au matuta, kutokana na matukio ya ajali za mara kwa mara za watu kugongwa katika barabara hiyo.

Wakazi hao wamesema wanawaomba Wakala wa Barabara. Tanzania (TANROADS) kuweka tuta eneo hilo kwa kuwa kuna shule karibu na eneo husika huku mistari ya pundamilia ipo mbali na hapo.

Diwani wa Kata ya Kitwiru, Dk Hamza Mumuhehe alipoulizwa amesemea kwa mujibu wa maelezo ya TANROADS kitaalamu eneo hilo ni ngumu kuweka tuta kwa kuwa kuna kona na mlima badala yake wakaweka matuta karibukaribu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live