Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilemela yapokea bilioni 46/- miradi ya maendeleo

Fedha Ed Ilemela yapokea bilioni 46/- miradi ya maendeleo

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi Dk Angeline Mabula amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Sh46 bilioni kwa miaka miwili.

Dk Mabula amesema hayo Julai 20, 2023 jijini Mwanza wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Wilaya ya Ilemela kwa kipindi cha mwaka 2020-2022 kwenye mkutano maalum wa wajumbe wa CCM wilayani humo.

‘’Hakika tunajivunia kuwa na rais mwenye maono mwenye kujali ustawi wa watu anaowaongoza kwa kuhakikisha huduma za jamii zinawafikia watanzania wote kwa wakati’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa Ilemela, katika kipindi cha miaka miwili Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela hadi kufikia Machi 2023 imepokea zaidi ya Sh46.089 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameitaja miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa ufanisi katika jimbo lake kuwa ni pamoja na sekta ya ardhi, afya, elimu, maji, miundommbinu, uvuvi, pamoja na masoko na biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live