Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu, Majimaji karata muhimu leo

Cae5580826e5d1663de9dd5cebfb1877 Ihefu, Majimaji karata muhimu leo

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU za Ihefu FC pamoja na Majimaji FC leo zina kibarua kikubwa cha kuhakikisha zinapata ushindi mnono katika hatua ya mtoano kuwania nafasi ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Ihefu itakuwa nyumbani katika Uwanja wa High Land Estate, Mbarali kuwaalika Transit Camp ambapo katika mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha mabao 3-0.

Ili kupata nafasi hiyo Ihefu inahitajika kupata ushindi wa zaidi ya mabao 3-0 huku wapinzani wao wakitafuta sare ya aina yoyote.

Majimaji ya Songea itakuwa ugenini kucheza na Geita Gold FC ambapo katika mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha mabao 2-1.

Geita nao watahitaji kupata sare ya aina yoyote ili kuipata nafasi hiyo.

Washindi wa jumla wa michezo hii watakabiliana na timu za ligi kuu zilizoshika nafasi ya 15 na 16 kucheza mchezo wa mtoano ili kupata timu za kucheza ligi kuu na mshindwa wa jumla atabaki ligi daraja la kwanza.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Ihefu, Maka Mwalwisi alisema. “Kwa kuwa wapinzani wetu walitufunga mabao hayo kwenye uwanja wao wa nyumbani ndani ya dakika 90 na sisi pia tuna uwezo mkubwa wa kuzitumia dakika hizo vizuri tukiwa nyumbani na tukapata ushindi ambao utatuwezesha kusonga mbele,” alisema Maka.

Mechi za mtoano za kushirikisha timu za ligi kuu zitaanza kuchezwa Julai 29 na marudiano ni Agosti mosi na baada ya matokeo mshindi wa jumla kama ni timu ya ligi kuu atabaki ligi kuu na kama ni ligi daraja la kwanza atapanda ligi kuu.

Chanzo: habarileo.co.tz