Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na maji ya mafuriko Tanga yafikia 15

82096 Tanga+pic Idadi ya vifo vilivyosababishwa na maji ya mafuriko Tanga yafikia 15

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Idadi ya miili iliyopatikana kutokana na athari za mvua wilayani Handeni mkoani Tanga imefikia 15 baada ya mwili mwingine kupatikana leo Jumatatu Oktoba 28, 2019.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amethibitisha na kusema kuwa mwili huo umepatikana kwenye gari ambayo ilisababisha vifo vya watu 10 na kwa sasa idadi ya marehemu waliopatikana kwenye gari hiyo imefikia 11.

Amesema wanaendelea kufuatilia kwenye maeneo mbalimbali ambayo yanatajwa kuathirika hivyo kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi kwa kuheshimu alama zilizowekwa kwenye maeneo yote hatarishi.

Kamanda huyo amewataka wananchi kufuatilia miili ambayo bado ipo hospitali ya mji Handeni kwaajili ya kutambua marehemu hao.

“Tumeweka alama kwenye maeneo yote hatarishi, madereva wazingatie alama zilizopo ili kuweza kuepuka athari zaidi kwenye sehemu hizo,” amesema Bukombe.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji Handeni, Feisal Said amesema tangu kuanza kwa mvua hizo Oktoba 25 wamepokea maiti 12 kati ya hizo 10 zimetokana na ajali na nyingine ni wale waliosombwa na maji.

Pia Soma

Advertisement

Amesema zimebakia maiti mbili bado hazijatambuliwa ambapo kati hizo 9 ni wanawake wakiwemo watoto wawili na mbili walikuwa wanaume.

Wakati huohuo, mabwawa 11 yamesombwa na maji wilayani Handeni kutokana  na mvua hizo na kusababisha wananchi takribani 55,000 wanaoishi wilayani humo kukosa maji ya uhakika.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela ameiomba wizara ya maji kuhakikisha inachukua hatua za dharula kuyafanyia ukarabati haraka.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz