Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IMANI POTOFU: Hapi alia na Sangoma ubakaji wa watoto

41922 Pic+hapi IMANI POTOFU: Hapi alia na Sangoma ubakaji wa watoto

Sat, 16 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewaonya waganga wa kienyeji wanaowapotosha wateja wao kubaka watoto ili wapate utajiri kuwa watachukuliwa hatua kali ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Akizungumza kwenye kampeni ya ‘Jiongeze tuwavushe salama mama mjamzito na mtoto mchanga’ mjini hapa juzi, Hapi alisema baadhi ya waganga wa kienyeji wanawadanganya watu kuwa ili kusafisha nyota na kupata utajiri ni lazima kubaka mtoto.

“Haiwezekani kuwe na waganga 878 je wanatibu watu gani? Hawa ndiyo wanaosababisha ubakaji watoto wetu, nataka kujiridhisha kama kweli hawa ni waganga au ndio wanasababisha watoto kubakwa,” alisema.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire akitoa takwimu katika kikao kilichowakutanisha wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, viongozi wa dini, waganga wajadi, madaktari na watu mbalimbali alisema Januari hadi Desemba mwaka jana kesi za kubaka mkoani humo zilikuwa 239, kulawiti 31 na mimba za utotoni 149 na kwamba watuhumiwa wote walifikishwa kwenye vyombo vya sheria. “Watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani kwa sababu ya ukatili kwa watoto wadogo na kwa watu mbalimbali na sheria imechukua mkondo wake.”

Akichangia mada, mganga wa tiba asili, Galusi Msekwa mkazi wa Tanangozi alisema waganga wa kienyeji wanaopiga ramli wanatoka nje ya Iringa na kwamba ndiyo wanaosababisha watoto kubakwa kwa dhana potofu kwamba mtu akifanya hivyo atapata utajiri.

“Hakuna uweli wowote katika hilo bali kuna watu wana lengo lakujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu jambo ambalo linazua balaa katika maeneo yetu na kusababisha waganga wote kuonekaa matapeli,” alisema.

Naye mbunge viti maalumu Chadema, Suzana Mgonakulima alisema hatua stahiki zipaswa kuchukuliwa haraka ili kutokomeza jambo hili.



Chanzo: mwananchi.co.tz