Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP mstaafu Pundugu afariki dunia

Thu, 27 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu, Samweli Pundugu (90) amefariki dunia.

Akitoa taarifa za kifo hicho leo Septemba 26, 2018 jijini Dodoma, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa amesema IGP Pundugu amefariki dunia leo katika hospitali ya Kilwa Road, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es Salaam na kwamba Jeshi la Polisi nchini litaendelea kutoa taarifa zaidi za msiba huo.

Amesema IGP Pundugu alizaliwa mwaka 1928 na alikuwa ni IGP wa pili nchini ambapo aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 1973 hadi mwaka 1975

Amesema aliajiriwa na Jeshi la Polisi tangu mwaka 1949 baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari katika Shule ya Wavulana Tabora.

Chanzo: mwananchi.co.tz