Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Sirro atarajia kufanya ziara Manyara

Siro Ed IGP Sirro atarajia kufanya ziara Manyara

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo Juni 30, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merrisone Mwakyoma amesema ziara hiyo itakuwa Julai 3, 2021 na atapata fursa ya kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni viongozi wa dini, wazee, wenyeviti wa vijiji, maofisa watendaji wa vijiji na wote wanaoshirikiana na polisi kufanikisha ulinzi shirikishi.

Mwakyoma amesema polisi hawawezi kumaliza uhalifu wenyewe bila kushirikiana na jamii kwa kuwa wahalifu wapo mitaani na wanaishi nao.

"Mara nyingi ushirikiano wa jamii unafanikisha kazi ya polisi na tunapowaelewesha watueleze nasi tunatunza siri kwa watoa taarifa na kuendelea kushirikiana,"

"Wakati mwingine jamii hulaumu polisi kuwa uhalifu umezidi wakati mwananchi huyo hawajibiki kutoa taarifa pindi anapobaini viashiria vya uhalifu katika eneo lake," amesema Mwakyoma.

Chanzo: ippmedia.com