Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Sirro ampandisha cheo polisi aliyekataa kupokea rushwa

89590 Sirro+pic IGP Sirro ampandisha cheo polisi aliyekataa kupokea rushwa

Mon, 23 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amempandisha cheo sajenti  Meshack Samson kuwa stafu sajenti na kumzawadia Sh1 milioni baada ya kukataa kupokea rushwa ya Sh10 milioni.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo Jumapili Desemba 22, 2019  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema askari huyo aliombwa kupokea Sh10 milioni ili afute tuhuma alizokuwa akizifuatilia.

"Tumewakamata watuhumiwa wawili wakishirikiana na Polisi wetu kutaka kumpa rushwa sajenti Meshack ili kumaliza kesi inayomkabili ndugu yao, hili jambo halikubaliki kabisa katika jeshi letu," amesema Shana.

Chanzo: mwananchi.co.tz