Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IDFA yapata viongozi wapya

Ecf65664394ef3efe5e9bf36d511f7fd IDFA yapata viongozi wapya

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha soka wilaya ya Ilemela(IDFA ) jijini Mwanza kimepata viongozi wapya wa chama hicho. Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi,Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Bittony Mwakisu alisema jumla ya Idadi ya wapiga kura walikuwa 67.

Mwakisu alisema katika nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho kulikuwa na mgombea mmoja Ephraim Majinge. Alisema Majinge ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura za ndiyo 67 na hakuna kura iliyoharibika.

Alisema katika nafasi ya katibu Mkuu Almas Moshi aliibuka mshindi baada ya kupata kura za ndiyo 67 huku Mohamed Badru alishinda nafasi ya mweka hazina baada ya kupata kura za ndio 63. Mwakisu alisema nafasi ya mwakilishi wa vilabu alishinda Kenedy Mangure kwa kupata kura za ndio 65 na nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu alishinda Jackson Fundi baada ya kupata kura za ndio 65.

Alisema nafasi ya mjumbe wa kamati tendaji alishinda Mussa Selemani kwa kura za ndio 66 na Hilda Mapunda alishinda kwa kupata kura za ndio 67. Mwenyekiti aliemaliza muda wake Evarist Agila alisema anawapongeza viongozi wapya na aliaahidi kuhakikisha anashirikiana nao wakati wote.

Alisema ataendelea kuvisaidia vilabu vyote vya Ilemela na aliahidi atalipa laki moja kwa vilabu vyote kwajili ya viingilio kwa ligi daraja la nne.

Aliahidi atatoa shilingi milioni 3/- kwa viongozi wapya kwajili ya ujenzi wa ofisi. Mwenyekiti mpya wa IDFA,Ephraim Majinge alisema atahakikisha anahakikisha vilabu vyote wilayani Ilemela vinasajiliwa.

Majinge alisema atahakikisha anaongeza idadi ya waamuzi na makocha kwa kuletea fursa za fani hizo wilayani Ilemela. Katibu mkuu wa IDFA,Almas Moshi alisema atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha mpira wilayani Ilemela unachezwa.

Chanzo: habarileo.co.tz