Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma ya mtoto njiti sasa ni uhakika

Watoto Njiti Huduma ya mtoto njiti sasa ni uhakika

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya Kigamboni, Halima Bulembo amepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kuanzisha wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) kwenye hospitali ya wilaya hiyo kutoka Taasisi ya Doris Mollel.

“Tumefuta kauli ya hakuna vifaa, kwa sasa hatutakuwa na rufaa, tumeletewa msaada huu wenye thamani kubwa, turudishe dhumuni la wasamaria wema waliochangia kupitia Taasisi ya Doris Mollel. Kwa sasa tukizungumzia watoto njiti tunajivunia kazi nzuri mnayoifanya na Doris Mollel,” amesema Bulembo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dkt. Lucas Ngawitu amesema watoto njiti 54 wamezaliwa katika wilaya hiyo kuanzia Januari mpaka sasa na wote walipewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live