Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma mji wa Mtumba kuanza Januari

Mkoa Wa Dodoma Wazindua Mradi Wa Afya Ya Uzazi Kwa Vijana Na Wanawake Huduma mji wa Mtumba kuanza Januari

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa awataka wakandarasi wanaojenga Mji wa Serikali Mtumba, kukamailisha kazi hiyo haraka ili ifikapo Januari mwakani, Serikali iwezi kuanza kazi rasmi katika eneo hilo.

Amesisitiza kwa hatua zilizopo sasa za umaliziaji zinataka ubora ambao utakuwa na sura ya Mji wa Serikali.

Senyamule ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kikazi hapa Mtumba ambapo aliongozana na kamati ya usalama ya mkoa pamoja na makatibu wakuu wa ofisi ya Rais Utumishi.

"Nitoe shime kwa Wakandarasi waliopata bahati kujenga majengo ya Serikali waharakishe umaliziaji ili wakabidhi kama agizo la Waziri Mkuu lililotaka ofisi zikabidhiwe mwisho wa mwaka," amesema.

Vilevile amesema huo ni sehemu ya maendeleo ya Dodoma kwa kuwa kwa Afrika Mashariki upo Tanzania pekee na kwamba utakuwa sehemu ya sehemu ya utalii mkoani humo.

Akiwa kwenye jengo la Utumishi linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), Senyamule na timu yake amesema wananchi wanataka kupata huduma za kiserikali hivyo wakandarasi wanapaswa wafanye umaliziaji haraka kama walivyoahidi.

"Kuna majengo yamefikia asilimia 90, mengine 73-78 ni kati ya majengo yaliyotakiwa yawe yamekamilika. Ziko changamoto zinazoweza kutatulika. Hivyo nitoe wito kwa wakandarasi kujenga mji huu ambao ni kielelezo kikubwa cha nchi kukamilisha kwa wakati," amesema.

Aidha amebainisha kuwa kutakuwa na wageni watakaokuja kupata huduma na wengine kuuangalia mji huo wakitaka kujua unafananaje, na kwamba Serikali ina haraka kwa kuwa inapotoa fedha inataka hatua zikamilike kwa wakati.

"Ninyi mnaojenga hili jengo la Utumishi niwapongeze mmekuwa mfano tunataraji kabla ya Desemba mtakuwa mmekabidhi," amesema Senyamule.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi, Xavier Daudi amesema matamanio yao ni kuhakikisha Januari 1, 2024 watakuwa wameshahamia tayari kuanza kutoa huduma kwa wananchi hivyo wanahimiza wakandarasi kumaliza ndani ya muda ulioahidiwa.

"Tunakuahidi Novemba 30, jengo litakuwa limeshakamilika na kukabidhiwa. Dhamana tuliyopewa ni ya utumishi wa umma hivyo tunaamini jengo likiwa hapa huduma zitawarahisishia wapokea huduma wetu," amesema.

Akipokea maelekezo hayo ya Mkuu wa Mkoa, Meneja wa Ujenzi TBA inayojenga jengo hilo la Utumishi, Mhandisi Manase Shekalaghe, amesema wamejipanga vyema kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda ulioahidiwa.

"Tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunakamilisha mradi kwa wakati kwa kuzingatia ubora. Tumejipanga kuhakikisha Novemba 30 tunakabidhi mradi huu," amesema Shekalaghe.

Amesema kwa sasa kazi zilizobaki ni umaliziaji (finishing), kwakuwa sehemu kubwa ya mradi imeshamalizika.

Hata hivyo amesema wanafuatilia kwa karibu vifaa wanavyovingoja ili kumaliza kulingana na malengo tatajiwa ya mradi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live