Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima, ametoa muda siku saba kwa hospitali zote nchini kukamilisha taarifa za utekelezaji wa mpango maalum wa watoto wachanga Nest 360 kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Amebainisha hayo wakati akizindua mpango maalumu wa utekelezaji wa watoto wachanga Nest 360 katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Temeke Jijini Dar es salaam ambayo imeboresha huduma kwa kihudumia watoto kutoka watoto 20 Mwaka 2019 hadi kufikia watoto 70 mwaka 2021 kwa siku hali iliyopunguza msongamano katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha amewataka watumishi wote wa afya kuzingatia misingi na weledi wa kazi zao ili kuweza kufikiaalengo yaliyowekwa na Wizara hiyo ya kuboresha afya kwa kila mwananchi.