Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali yakanusha kukataa kumhudumia mgonjwa

Kisarawe Web Hospitali yakanusha kukataa kumhudumia mgonjwa

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya wilaya ya Kisarawe imekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mgonjwa aitwaye Batholomeo Mapunda mkazi wa Temeke, alifukuzwa na kushindwa kufanyiwa upasuaji hospitalini hapo kwa kukosa shilingi laki mbili na elfu hamsini si za kweli.

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt. Zaitun Hamza, amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani taarifa hiyo ilianza kuzagaa mitandaoni Agosti 21, 2022, ili hali mgonjwa alifanyiwa upasuaji Agosti 18, mwaka huu.

Mganga Mkuu huyo amesema mgonjwa alifika hospitalini hapo Agosti 14, akiwa na hernia na akafanyiwa matibabu ya awali kisha akaruhusiwa na kupewa taratibu zote kwa ajili ya  kufanyiwa upasuaji na kwamba alitakiwa alipie gharama ya upasuaji ambayo ni shilingi elfu 50 tu na si shilingi laki mbili na hamsini iliyoripotiwa kwnye mitandao hiyo ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live