Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Karagwe yaanza kufanya upasuaji

MOI Yafanya Upasuaji Wa Kuondoa Uvimbe Kwa Kutumia Pua Hospitali ya Karagwe yaanza kufanya upasuaji

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wananchi 23,000 waishio katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na maeneo jirani wataondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za upasuaji, baada ya hospitali ya halmashauri hiyo kuanza kutoa huduma hiyo hii leo.

Hospitali hiyo iliyoanza kujengwa mwaka 2019 na kukamilika mwaka 2020, imejengwa kwa gharama ya Sh3.4 bilioni huku ikiwa na majengo 14 na watumishi 45.

Zawadi Jackson ambaye amekuwa mwananchi wa kwanza kupata huduma hiyo hospitalini hapo leo Septemba 12, 2023 ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa huduma hiyo.

“Kwanza nashukuru nimehudumiwa vizuri na mimi pamoja na mwanangu tunaendelea vizuri. Napenda kuishuru sana Serikali kwa kutuletea hii huduma hapa kwetu. Sisi kina mama tulikuwa tunatembea umbali mrefu kufuata hii huduma Bukoba mjini na sehemu nyingine. Tunaomba tuzidi kuletewa huduma nyingine zaidi,” amesema.

Upasuaji huo wa kwanza hospitalini hapo umefanywa na na madaktari Dk Karimu Abdalah, Dk Mugisha Laurian wakishirikiana manesi Irene Mlekio, Lydia Kanyinginya mtaalamu wa usingizi, alikuwa ni Oscar Kilengule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live