Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali Njombe yatoa huduma za CT-scan, operesheni

Upasuaji Upoasuaji Mtoito.png Hospitali Njombe yatoa huduma za CT-scan, operesheni

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe imeanza kutoa huduma ambazo awali ilikuwa hazitolewi ikiwemo CT Scan na oparesheni za kitaalamu zinazofanywa na wataalam walioajiriwa katika hospitali hiyo.

Hayo yameelezwa jana Julai 26 na ofisa tawala wa wilaya hiyo, Watson Kisinini alipozungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya, Kissa Kasongwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/23 wilayani humo.

Amesema kutokana na utoaji wa huduma hizo madiwani wanatakiwa kuwa mabalozi kwa kutoa taarifa kwa wananchi ili waweze kwenda kupatiwa huduma hizo.

Amesema huduma hizo awali zilikuwa zinapatikana katika hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete, hivyo kusogea kwa huduma mpaka hospitali hiyo ya rufaa kutapunguza gharama na umbali kwa wananchi.

"Tunaomba hili tangazo lifike kwa wananchi ili walitambue hilo ili wasiendelee kwenda umbali huo wakati huduma waliyokuwa wanaifuata Ikonda hata hapa wanaweza kuipata,” amesema Kisinini.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Filoteus Mligo amesema madiwani watatekeleza agizo hilo la kuwaeleza wananchi juu ya upatikanaji wa huduma hizo ambazo zimesogezwa karibu tofauti na mwanzao ambapo zilikuwa zinapatikana umbali mrefu.

"Nashukuru kwa hotuba yako ambayo mengi ni maagizo ya kuisemea vizuri hospitali yetu ya rufaa na huduma zinazotolewa pale ili wananchi wajue kinachoendelea," amesema Mligo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live